top of page

Kiswahili

KARIBU!

Karibu kwenya Bismarck Global Neighbors, na asante kwa maslahi yako. Hapa global neighbours tunapenda kukuita jirani wetu mpya. Labda umefika tu USA kama mkimbizi au umekuja kwa kibali ya kufanya kazi ama umeishi katika usawa wa maisha yako hapa lakini uko mgeni hapa Bismarck. Unaeza kua rahia wa America lakini una shida na lugha ya kiengereza.

Hata hivyo tunafurahiya kuja kwako. Uwepo wako unafurahisha jumuiya yetu yote. Tunataka kukusaidia kustawi na kujiskia nyumbani.

 

JINSI YA KUKUSAIDIA

 

Mpango wetu wa mshauri wa bure inakulinganisha wewe au familia yako na muamerikani  ambaye amejitotelea kukusaidia na lugha ya kiengereza, swala ya shule, maombi ya kazi, utamaduni,kupata kufahamu North Dakota, na kuendesha gari. Mtu huyu ni kama mwalimu na rafiki ambaye anataka ufanikiwe hapa USA. Na wewe umjulishe utamaduni ya kwenu nyumbani na hadithi, kusaidia jumuiya yetu kukukaribisha zaidi.

Kuwa na mshauri ni bure, ila kusikizana nawe kukuona mara moja kwa wiki kwa muda wa miezi sita.Pamoja mtakua na lengo kwa kufanya maisha bora hapa North Dakota. Mnaeza kukutana kwa nyumba zenu au kwenye jumuiya. Unaeza omba uwe na mtu wa jinsia yako au kukamilisha huu mipango kwa wakati wowote.

 

Tafadhali jaza fomu hii ukitaka mshauri.

Kwa maswali tuma barua pepe kwenye anwani  bismarckglobalneighbours@gmail.com au piga simu kwenye nambari 701-595-0135 na wattsup.

Tembelea tovuti yetu www.bismarckglobalneighbours.org kwa mengi kuhusu mshauri

bottom of page